Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 10 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 152 2023-11-10

Name

Amina Ali Mzee

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AMINA ALI MZEE aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kuliwezesha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kujiendesha kibiashara?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Amina Ali Mzee, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mkakati wa Serikali ni kuhakikisha Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) linatekeleza majukumu yake kikamilifu kama chombo cha utangazaji cha umma. Serikali ipo katika mkakati wa kukamilisha utungaji wa Sheria ya TBC ya mwaka 2023, itakayowezesha kuwa na vyanzo vya uhakika vya mapato. Aidha, TBC inazo chaneli za kimkakati kwa ajili ya kuongeza mapato ikiwemo TBC2, TBC Online, TBC FM na Radio za Jamii Dodoma na Arusha, ahsante.