Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 53 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 464 2022-06-28

Name

Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itajenga kingo za Mto Kanoni unaopita katikati ya Mji wa Bukoba?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Oliver Daniel Semuguruka, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Halmashaurii ya Manispaa ya Bukoba mwezi Februari, 2022 ilitumia shilingi milioni sita kupitia mapato ya ndani kwa ajili ya kusafisha, kupanua na kuongeza kina cha Mto Kanoni.

Mheshimiwa Spika, ili kuondoa changamoto hiyo Serikali katika mwaka wa fedha 2022/2023 imejumuisha mradi wa ujenzi wa kingo za Mto Kanoni kwenye Mpango wa TACTIC Awamu ya Pili unaotarajiwa kuanza mwezi Januari, 2023, ahsante.