Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 53 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 471 2022-06-28

Name

Juliana Daniel Shonza

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE K.n.y MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa kituo cha Polisi Mji Mdogo wa Mlowo baada ya kilichopo kuwekewa alama ya kubomolewa?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Juliana Shonza, Mbunge wa Viti maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali itaanza ujenzi wa kituo cha Polisi Mji Mdogo wa Mlowo baada ya Halmashauri kuzingatia na kutekeleza maagizo ya Kamati ya Usalama ya Mkoa ambayo ni kupata eneo la kutosha, kujenga kituo na nyumba za Askari, Wakaguzi na Maofisa na kuandaa Hati Miliki ya eneo litakalopatikana.