Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

George Ranwell Mwenisongole

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbozi

Primary Question

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE K.n.y MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa kituo cha Polisi Mji Mdogo wa Mlowo baada ya kilichopo kuwekewa alama ya kubomolewa?

Supplementary Question 1

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri lakini naomba commitment ya Mheshimiwa Waziri.

Je, uko tayari kuongozana na sisi kwenda Mbozi kuangalia hali ya vituo vya Polisi na kuhusu ujenzi wa hicho kituo?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mwenisongole kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nimepokea ombi lake na ninamuahidi Mheshimiwa Mbunge kwamba baada ya kujibu swali hili tutakaa tupange ratiba mimi na yeye ya kuweza kutembelea kwenye Jimbo lake ili kuweza kukagua maendeleo ya vyombo vyetu vya usalama vilivyopo chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani kwa ujumla wake.

Name

Deodatus Philip Mwanyika

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Njombe Mjini

Primary Question

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE K.n.y MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa kituo cha Polisi Mji Mdogo wa Mlowo baada ya kilichopo kuwekewa alama ya kubomolewa?

Supplementary Question 2

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, katika Mkoa wa Njombe hatuna Kituo cha Polisi ambacho kina hadhi ya Mkoa Polisi wanakaa kwenye nyumba mbalimbali ambazo zimetawanyika.

Je, ni lini sasa Serikali ina mpango wa kujenga kituyo kipya chenye hadhi ya Kimkoa?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Deodatus Mwanyika Mbunge wa Njombe Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ninamhakikishie Mheshimiwa Mbunge pamoja na Waheshimiwa Wabunge wote ambao katika maeneo yao hakuna vituo vya Polisi, kwamba Serikali tumeanza jitihada hizo za kuhakikisha kwamba tuna kamilisha ujenzi wa Vituo vya Polisi katika ngazi zote kuanzia ngazi ya Mikoa, Wilaya, Kata.

Mheshimiwa Spika, nilipokuwa nimewasilisha bajeti yangu ya Wizara yangu mwaka huu wa fedha niliainisha juu ya mpango huo kabambe wa Serikali wa miaka 10, ambao utahusisha ujenzi wa nyumba za Askari pamoja na vituo vya Polisi zaidi ya 51,000 nchi nzima.

Kwa hiyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba viko vituo ambavyo tutaanza navyo mwaka huu wa fedha na vingine vitafuata baadaye ikiwemo katika Jimbo la Mheshimiwa Mbunge aliyeuliza swali.

Name

Noah Lemburis Saputi Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE K.n.y MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa kituo cha Polisi Mji Mdogo wa Mlowo baada ya kilichopo kuwekewa alama ya kubomolewa?

Supplementary Question 3

MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Spika, naomba kuuliza swali moja kwamba Mji Mdogo wa Ngaramtoni katika Jimbo la Arumeru Magharibi umekuwa Mji Mkubwa kidogo na hauna Kituo cha Polisi chenye hadhi, inatumia nyumba ya Mtumishi wa Shamba la Mbegu.

Je, ni lini Serikali itajenga Kituo cha Polisi katika Mji Mdogo wa Ngaramtoni?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kama alivyozungumza Mheshimiwa Mbunge kwamba Mji wa Ngaramtoni hakuna kituo cha Polisi, hivyo kwanza nipongeze jitihada zilizochukuliwa na hasa za Mwananchi aliyejitolea kutoa jengo kwa ajili ya matumizi ya kituo cha Polisi.

Ninamuomba Mheshimiwa Mbunge kwamba jambo hili nilichukue ili tuone jinsi gani tunaweza kufanya kutatua changamoto hii, ikiwezekana kuangalia jitihada mbalimbali kwa kushirikiana nae Mheshimiwa Mbunge ya kuanza ujenzi wa Kituo cha Polisi katika eneo hili.

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE K.n.y MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa kituo cha Polisi Mji Mdogo wa Mlowo baada ya kilichopo kuwekewa alama ya kubomolewa?

Supplementary Question 4

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ili niulize swali dogo la nyongeza.

Je, ni lini Wilaya ya Kilolo itajengewa ofisi ya Makao Makuu ya Polisi kwa sababu ni muda karibu miaka 20 haijajengewa Makao yalipo Makuu ya Wilaya?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, jibu la swali hili linafanana na jibu ambalo nilijibu katika swali la mwanzo juu ya mikakati na jitihada za Serikali za kutatua changamoto za vituo vya Polisi katika ngazi mbalimbali ikiwemo Wilaya ya Kilolo. Kwa hiyo, nimuombe Mheshimiwa Mbunge avute subira wakati jitihada hizo zikiwa zinaendelea.(Makofi)

Name

Asha Abdullah Juma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE K.n.y MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa kituo cha Polisi Mji Mdogo wa Mlowo baada ya kilichopo kuwekewa alama ya kubomolewa?

Supplementary Question 5

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

Kwa kuwa, uhitaji wa ujenzi wa vituo vya Polisi umekuwa mkubwa nchini; je, Serikali haioni umuhimu wa kuimarisha kikosi cha ujenzi cha Jeshi la Polisi na kuiga mfano kama wa Jeshi la Kujenga Taifa na Magereza katika ujenzi wa majengo yao, ambao pia utaokoa fedha nyingi za Serikali? (Makofi)

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Asha Abdallah Juma kama ifuatavyo:-

Swali zuri la Mheshimiwa Mbunge, ni kweli kuna umuhimu huo lakini umuhimu huo tumeshaanza kuuona na kuufanyia kazi, kwa maana ya kwamba kupitia Shirika letu la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi tumeanza jitihada za kuweza kufanya mageuzi makubwa ya shirika hili ili kuhakikisha linatoa mchango wake mkubwa katika kuendeleza miradi mbalimbali ya Jeshi la Polisi ikiwemo ya ujenzi.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie kwamba moja katika mikakati hiyo ni kuimarisha kikosi chetu cha ujenzi ambacho hata hivyo hakiko katika hali mbaya sana, kwa sababu ziko shughuli ambazo zinafanywa na kikosi cha ujenzi cha Jeshi la Polisi, lakini nakubaliana na yeye kwamba kuna haja ya kufanyakazi ya ziada zaidi kukiimarisha kiwe bora Zaidi. Hilo jambo tunaendelea nalo na wazo lake tutaendelea kulifanyia kazi.(Makofi)

Name

Flatei Gregory Massay

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbulu Vijijini

Primary Question

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE K.n.y MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa kituo cha Polisi Mji Mdogo wa Mlowo baada ya kilichopo kuwekewa alama ya kubomolewa?

Supplementary Question 6

MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa nafasi.

Jimbo la Mbulu Vijijini Kata ya Yaeda Chini ulikuja Mheshimiwa Waziri ukatuhamasisha tukajenga Kituo cha Polisi, sasa nguvu za wananchi pamoja na mimi tumeshindwa kujenga nyumba za Polisi. Utatusaidiaje kwenye bajeti hii ili nyumba hizo zipate kujengwa?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli mimi na yeye wakati nikiwa Naibu Waziri wa Wizara hii miaka kadhaa iliyopita tulishirikiana kuanza ujenzi wa kituo hiki. Kwa hiyo nichukue fursa hii kumpongeza yeye na wananchi wa Jimbo hilo kwa kuweza kutumiza ile ndoto tuliyokuwa nayo wakati tunaanza ujenzi huo na sasa hivi kituo kimekamilika.

Kwa hiyo nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba nguvu hizo za wananchi na nguvu zake hatuwezi kuziacha hivi hivi. Tumechukua suala la ujenzi wa Nyumba za Askari katika eneo hilo kwa uzito unaostahili na mimi nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kama tuliweza mimi na yeye kuanza jitihada za ujenzi wa kituo hicho, hatutashindwa mimi na yeye tukishirikiana kujenga Nyumba za Askari.

Name

Subira Khamis Mgalu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GEORGE R. MWENISONGOLE K.n.y MHE. JULIANA D. SHONZA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa kituo cha Polisi Mji Mdogo wa Mlowo baada ya kilichopo kuwekewa alama ya kubomolewa?

Supplementary Question 7

MHE. SUBIRA K. MGALU: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza.

Kwanza naishukuru Serikali kwa ukarabati wa ofisi ya kituo kidogo cha Polisi Jimbo la Chalinze.

Kwa kuwa, Wilaya yetu ya Bagamoyo ofisi ya Polisi majengo yake ni ya muda mrefu na yamechakaa na kwa kuwa tunatarajia watalii wengi kutokana na Royal Tour ambapo Mheshimiwa Rais alifika Bagamoyo.

Je, Serikali inatuahidi vipi katika kukarabati ofisi ya Polisi Wilaya ya Bagamoyo? Ahsante sana.

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-

Kwanza ninapokea pongezi kwa niaba ya Serikali juu ya kazi ambayo tayari imeshaanza kufanyika kama alivyoeleza Mheshimiwa Mbunge. Vilevile nichukue nafasi hii kutoa maelekezo kuwa tathmini ya ukarabati huo ufanyike ili tuweze kuangalia utaratibu wa kupata fedha kwa ajili ya kukarabati kituo hicho.