Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 2 | Planning and Investment | Ofisi ya Rais: Mipango na Uwekezaji | 20 | 2024-04-03 |
Name
Muharami Shabani Mkenge
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bagamoyo
Primary Question
MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE K.n.y. MHE. MUHARAMI S. MKENGE aliuliza: -
Je, lini Serikali itaachia maeneo yaliyotwaliwa na EPZA ambayo hayapo kwenye mipango ya matumizi ili wananchi wayatumie?
Name
Prof. Kitila Alexander Mkumbo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ubungo
Answer
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS MIPANGO NA UWEKEZAJI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mamlaka ya EPZA imetwaa maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kuanzisha Kanda Maalum za Kiuchumi. Maeneo hayo yapo katika hatua mbalimbali za utwaaji na uendelezaji. Katika kuendeleza maeneo hayo Mamlaka huandaa Mpango Kabambe ili kuainisha matumizi mbalimbali ya maeneo hayo. Hivyo, maeneo yaliyotwaliwa na EPZA bado yapo kwenye mpango wa matumizi yaliyokusudiwa.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved