Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Alice Karungi Kaijage

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE K.n.y. MHE. MUHARAMI S. MKENGE aliuliza: - Je, lini Serikali itaachia maeneo yaliyotwaliwa na EPZA ambayo hayapo kwenye mipango ya matumizi ili wananchi wayatumie?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa sasa ni mwaka wa 14 toka wananchi hawa wafanyiwe tathmini hawajalipwa, je, ni lini Serikali italipa wananchi hawa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; je, Waziri yupo tayari kuongozana na Mheshimiwa Mkenge, Mbunge wa Bagamoyo kwenda kuongea na hawa wananchi kujua hatma ya malipo yao? Ahsante. (Makofi)

Name

Prof. Kitila Alexander Mkumbo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ubungo

Answer

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS MIPANGO NA UWEKEZAJI: Mheshimiwa Spika, maeneo yote ambayo yametwaliwa yanayostahili kulipiwa fidia huwa tunaingiza kwenye bajeti na hata katika bajeti ambayo tutawalisha mwaka huu tutayapangia. Baadhi ya maeneo ambayo Mheshimiwa Mbunge anayataja yatakuwemo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu kwenda Bagamoyo Mheshimiwa Mkenge anafahamu kwamba hata mwaka jana tulikuwa naye na mwaka huu pia tumepanga kutembelea eneo la Bagamoyo. Kwa hiyo, wakati wowote tukimaliza vikao vya Bunge tutakwenda Bagamoyo. Ahsante sana.