Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 13 Sitting 4 Regional Administration and Local Government Authorities Wizara ya Viwanda , Biashara na Uwekezaji 110 2023-11-08

Name

Nicholaus George Ngassa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Igunga

Primary Question

MHE. NICHOLAUS G. NGASSA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itapandisha hadhi Shule ya Sekondari ya Igurubi iliyopo katika Wilaya ya Igunga kuwa ya kidato cha tano na cha sita?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE DEOGRATIUS J. NDEJEMBI) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Nicholaus George Ngassa, Mbunge wa Jimbo la Igunga kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kati ya shule zilizopendekezwa katika Tarafa ya Igurubi kuwa shule za A level ni Igurubi Sekondari na Mwamakona Sekondari. Suala lililokwamisha shule ya Igurubi kutosajiliwa ni kutokuwa na miundombinu Kama bweni, bwalo na miundombinu mingine wezeshi. Hivyo shule ikikidhi vigezo kwa mujibu wa miongozo na taratibu, itasajiliwa kuwa ya Kidato cha Tano na Sita.