Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 12 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 203 2024-02-14

Name

Justin Lazaro Nyamoga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilolo

Primary Question

MHE. JUSTIN L. NYAMOGA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itafunga mitambo ili wananchi wa Tarafa ya Kilolo wapate matangazo ya Redio ya Taifa (TBC)?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Justin Lazaro Nyamoga, Mbunge wa Kilolo, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Tarafa ya Kilolo ni miongoni mwa maeneo yaliyo katika miradi ya maendeleo yaliyopangwa kutekelezwa kwa mwaka 2023/2024 ambayo utekelezaji wake umeishaanza kwa hatua za utafiti wa kitaalam, kutangazwa na kufanyiwa tathmini kwa zabuni za ujenzi wa vituo na ununuzi wa mitambo ya vituo 14 ikiwemo Kilolo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mradi huu utatekelezwa katika Eneo la Ipugulu, Kijiji cha Lulanzi Kata ya Mtitu katika Tarafa ya Kilolo na umepangwa kukamilika ifikapo Juni, 2024.