Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 2 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 25 2024-04-03

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya zao la muhogo kuwa moja ya zao la kimkakati katika Mikoa ya Kusini?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yahya Ally Mhata, Mbunge wa Jimbo la Nanyumbu, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo inatekeleza mikakati mbalimbali ya kuendeleza zao la muhogo nchini. Mikakati hiyo ni pamoja na matumizi ya mbegu bora za muhogo zilizogunduliwa na TARI zenye uwezo wa kuzalisha tani 20 hadi 50 kwa ekari. Mbegu hizo zinapatikana kwenye Vituo vya Utafiti wa Kilimo (TARI) na kwa wazalishaji wa mbegu katika madaraja yote.

Mheshimiwa Spika, aidha, mbegu hizo zina sifa za mavuno yenye tija, wanga, kustahimili ukame, wadudu na ukinzani wa magonjwa. Kutokana na matumizi ya mbegu hizo, uzalishaji wa muhogo mkavu umeongezeka kutoka tani 2,486,000 Mwaka wa Fedha 2020/2021, hadi kufikia 2,575,453 Mwaka wa Fedha 2022/2023. Mkoa wa Mtwara upo katika nafasi ya tano ukitanguliwa na Tanga, Kigoma, Pwani na Kagera.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeandaa Mkakati Mahsusi wa Kuendeleza Zao la Muhogo nchini ambao unalenga kuhamasisha uzalishaji wa zao hilo kwa tija, upatikanaji wa masoko ya uhakika ya bidhaa za muhogo, kuhamasisha wawekezaji wa viwanda vya kuzalisha bidhaa za muhogo zenye thamani kubwa, kama vile viwanda vya kuzalisha wanga utokanao na zao la muhogo, bidhaa ambayo kwa sehemu kubwa huingizwa kutoka nje ya nchi.

Mheshimiwa Spika, aidha, kama sehemu ya utekelezaji wa mkakati huo, Wizara imepanga kufanya Cassava Business Forum ili kujadili biashara ya muhogo nchini utakaofanyika tarehe 15 Aprili, 2024. Kongamano hilo litawezesha kutangaza fursa zilizopo katika Mikoa ya Kusini.