Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. YAHYA A. MHATA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kufanya zao la muhogo kuwa moja ya zao la kimkakati katika Mikoa ya Kusini?

Supplementary Question 1

MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, changamoto kubwa ya wakulima wa zao la muhogo ni upatikanaji wa masoko. Nashukuru Mheshimiwa Waziri ameeleza, sasa je, katika hiyo Business Forum ambayo inategemea kufanyika mwezi huu, Waziri yupo tayari kuwaaalika wakulima wa muhogo kiutoka Jimbo la Nanyumbu ili washiriki, waje kueleza changamoto na matatizo yanayowakabili? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili; tumeona wadau wengi ambao kule kusini walikuwa wanashirikiana na Serikali sasa hivi hawapo na wameondoka katika maeneo yao. Je, ni sababu zipi ambazo zimewasababisha wadau wale VSO, TILED wameondoka katika maeneo ya Wilaya ya Nanyumbu na hawajulikani wako wapi? (Makofi)

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la kwanza, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika hiyo Casava Business Forum tutaalika wadau karibu wote ambao wanahusika na hii biashara ya muhogo wakiwemo wakulima wanaotoka eneo la Nanyumbu, kwa hiyo hilo naamini litafanyika.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili, sababu kubwa ambayo wadau hawa walikuwa wameondoka katika Jimbo la Nanyumbu, ilikuwa ni changamoto kubwa ya soko kama ambavyo tumejadili hapo na ndiyo maana unaona tunaitisha hii ili tuweze kujua namna bora ambapo tutaondokana na hizi changamoto ikiwemo kutafuta soko la uhakika na kuhamasisha uwekezaji wa zao la muhogo hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, haya yote tutayajibu zaidi kwenye hiyo forum na tutakuwa na mkakati madhubuti wa kuhakikisha sasa hizi changamoto zinazotokana na zao hili ambazo tumeweka katika mazao 15 ambayo tunaendanayo kimkakati zinaondoka. Ahsante sana.