Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 5 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 77 2024-02-05

Name

George Natany Malima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka vitendea kazi kama vile magari na pikipiki katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Mpwapwa?

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi napenda kujibu swali la Mheshimiwa George Natany Malima, Mbunge wa Mpwapwa, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Polisi Wilaya ya Mpwapwa ina magari mawili yanayohudumia Wilaya hiyo ambayo ni PT 3759 na PT 1975 Toyota Land Cruiser Pickup pamoja na pikipiki nne. Kwa kuwa magari na pikipiki hizo bado hazikidhi mahitaji, Serikali itaendelea kutenga fedha za kununua vitendea kazi hivyo kwa ajili ya Jeshi la Polisi na kuvigawa kwenye maeneo yenye changamoto kama Wilaya ya Mpwapwa. (Makofi)