Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

George Natany Malima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka vitendea kazi kama vile magari na pikipiki katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Mpwapwa?

Supplementary Question 1

MHE. GEORGE N. MALIMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza; utaratibu wa Serikali wa kupeleka Polisi Jamii karibu katika kila Kata umeonesha mafanikio makubwa. Usalama wa wananchi na mali zao umeimarika; je, ni lini Serikali itapeleka Polisi Jamii katika Kata zote za Jimbo la Mpwapwa? Hilo swali la kwanza. (Makofi)
Swali la pili; je, Serikali ina mpango gani kupeleka pikipiki kwa wale wachache ambao wako kwenye Kata chache za Jimbo la Mpwapwa ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao? (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali ya nyongeza ya Mheshimiwa George Malima, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu lini Polisi Jamii watapelekwa katika Kata zote za Jimbo la Mpwapwa ni kwamba, hayo ndiyo Maelekezo ya Serikali hususan Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, ambapo kupitia Jeshi la Polisi Mheshimiwa Rais ameridhia kutoa mafunzo kwa askari na ajira, kwa maana ya Wakaguzi Kata ili kuwezesha Kata zote kupata askari.

Mheshimiwa Naibu Spika, natumia jukwaa hili kumwelekeza IGP, ahakikishe kule ambapo hawajapangwa kama Mpwapwa kama ilivyoelezwa, basi kata zote zipate Askari Kata. Kwa sababu ajira zilizotolewa zinatosha kuziwezesha kata zote kupata Askari Kata kwa kiwango cha Mkaguzi wa Kata. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kuwapatia vitendea kazi, ni kwamba mwaka huu tunashukuru sana Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan na dhamira ya Mheshimiwa Rais mwenyewe, ameridhia kutoa zaidi ya shilingi bilioni 15 kwa ajili ya ununuzi wa magari 101 pamoja na pikipiki ili kuwezesha Wilaya, Mikoa ambayo haina magari pamoja na Kata kuweza kupata vitendea kazi hivyo. Mara pikipiki hizo zitakapopatikana Wilaya ya Mpwapwa pia itapelekewa, nashukuru. (Makofi)

Name

Samweli Xaday Hhayuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hanang'

Primary Question

MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka vitendea kazi kama vile magari na pikipiki katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Mpwapwa?

Supplementary Question 2

MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Wilayani Hanang halina vitendea kazi kabisa; je, Serikali ina kauli gani ili kuwapatia vitendea kazi hasa vya usafiri? (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tunafahamu na imeelezwa hapa wakati Mheshimiwa Waziri wangu akisoma Bajeti kwamba Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilikuwa na upungufu mkubwa wa vitendea kazi na ndiyo maana limekuwa likipata changamoto kuokoa kwenye maeneo yanayohitaji uokozi wa haraka.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kutambua hilo Serikali ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeridhia ku-process mkopo wa zaidi ya dola milioni 100 kwa ajili ya kuliwezesha Jeshi la Zimamoto kupata vitendea kazi na vifaa vingine ikiwemo magari, maana yake usafiri. Ili viweze kuwezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufasaha. Mara vitendea kazi hivyo vitakaponunuliwa, Jeshi hilo litapewa ikiwemo Wilaya yako ya Hanang. (Makofi)

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka vitendea kazi kama vile magari na pikipiki katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Mpwapwa?

Supplementary Question 3


MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, je, uko tayari kumuondolea udhalili OCD wa Nyang’hwale, kwa kupitisha bakuli kwa kuomba fedha kwa ajili ya kutengeneza gari lake ambalo siyo zuri na ni bovu? (Makofi)

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakiri kuwepo kwa baadhi ya OCDs kwenye Wilaya mbalimbali ambapo wana magari yaliyochakaa ikiwemo Wilaya ya Nyang’hwale. Kama nilivyosema kwenye jibu langu la msingi, magari yatakayonunuliwa kupitia shilingi bilioni 15 tulizopewa, vipaumbele ni Wilaya zisizokuwa na magari au magari yaliyochakaa sana ikiwemo Wilaya yake ya Nyang’hwale. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa Wilaya ya Nyang’hwale itapewa katika mgao huo. (Makofi)

Name

Boniphace Nyangindu Butondo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kishapu

Primary Question

MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka vitendea kazi kama vile magari na pikipiki katika Kituo cha Polisi Wilaya ya Mpwapwa?

Supplementary Question 4

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, Wilaya ya Kishapu ni moja kati ya Wilaya ambazo hazina magari kabisa na sasa hivi tunatumia gari moja la kuazimwa na Mgodi wa Williamson Diamond Limited; ni lini magari haya mapya yaliyotolewa na Serikali yataletwa katika Wilaya ya Kishapu ili kutatua tatizo kubwa lililopo katika Wilaya hiyo? (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, nimeshajibu kwenye maswali ya nyongeza yanayofanana na hili, labda niongeze maelezo ya ziada kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika hizi shilingi bilioni 15 zilizotolewa na Mheshimiwa Rais, tayari Hazina wameshatupatia shilingi bilioni 10.1 na tumenunua magari 30 kwa ajili ya OCDs lakini tumenunua magari kwa ajili ya RPCs wa mikoa 12 na mengine ya kuongozea misafara. Mara magari haya yatakapotolewa, nataka niwahakikishe Waheshimiwa Wabunge, Wilaya zote ambazo hazina magari, zitapata magari. Nashukuru. (Makofi)