Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 9 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 144 2024-02-09

Name

Ally Mohamed Kassinge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kusini

Primary Question

MHE. SAMWELI X. HHAYUMA K.n.y MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza: -

Je, mazungumzo kati ya Serikali na mwekezaji wa Kiwanda cha Mbolea Kilwa kuhusu gesi asilia ya Songosongo yamefikia hatua gani?

Name

Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Kondoa

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ally Mohamed Kassinge, Mbunge wa Kilwa Kusini, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na majadiliano na wawekezaji mbalimbali wakiwemo Kampuni ya HELM, FERROSTAAL na PolyServe ili kuharakisha uwekezaji wa kiwanda cha mbolea Kilwa Masoko.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali inaendelea kutangaza fursa ya uanzishwaji wa viwanda vya mbolea nchini ikiwemo eneo la Kilwa Masoko kutokana na uhitaji mkubwa wa mbolea hapa nchini.