Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 9 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 151 2024-02-09

Name

Selemani Jumanne Zedi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukene

Primary Question

MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kufufua Skimu za Umwagiliaji za Ikindwa, Malolo na Nhalanga – Bukene ili zifanye kazi kwa tija?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana na kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Selemani Jumanne Zedi, Mbunge wa Jimbo la Bukene, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Skimu za Umwagiliaji za Ikindwa yenye jumla ya hekta 1,000 na Malolo yenye jumla ya hekta 500, ni miongoni mwa skimu zilizotengewa fedha katika mwaka wa fedha 2023/2024 kupitia mpango wa bajeti ya Tume ya Taifa ya Umwagiliaji, kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ili kujua gharama halisi za ujenzi na uboreshaji wa skimu hizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea na zoezi la upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa skimu, mabwawa ya umwagiliaji, visima virefu kwa ajili ya umwagiliaji pamoja na mabonde mbalimbali ya umwagiliaji nchini, ikiwemo Bonde la Mto Manonga linaloanzia Shinyanga hadi Singida. Ninaomba nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge kwamba, katika kazi hii inayoendelea ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina, skimu tajwa hapo juu zitafikiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, kazi ya uboreshaji wa skimu hizo zitaanza kutekelezwa mara baada ya kukamilika kwa kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina ambapo gharama halisi ya uboreshaji itakuwa imejulikana. (Makofi)