Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 9 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 153 2024-02-09

Name

Sophia Hebron Mwakagenda

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaruhusu ushindani wa kibiashara kwenye mazao ya chai na maziwa Wilayani Rungwe?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Kilimo, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sophia Hebron Mwakagenda, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Kilimo kupitia Bodi ya Chai na Tume ya Maendeleo ya Ushirika inahamasisha wakulima wa chai kujiunga kwenye Ushirika ili waweze kuwa na sauti ya pamoja katika ufanyaji wa biashara ya zao la chai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Wilaya ya Rungwe, biashara ya majani mabichi ya chai hufanywa baina ya wakulima wadogo (wauzaji) na viwanda (soko). Wakulima hawa wako huru kuuza majani yao katika kiwanda chochote kulingana na masharti yaliyopo kwenye mikataba ya mauziano. Bodi ya Chai inasajili na kufanya usimamizi wa mikataba yote ya mauziano ya majani mabichi ya chai.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ushindani wa kibiashara katika mazao ya maziwa umeruhusiwa nchini, ikiwemo katika Wilaya ya Rungwe. Kwa sasa kuna kampuni sita zinazonunua maziwa katika Wilaya ya Rungwe ambayo ni ASAS Dairy, Mbeya Milk, Tanga Fresh, Njombe Milk, Full Manyoyo na Dodoma Halisi. Pamoja na kampuni hizo, kuna wanunuzi wengine wadogo wanaonunua maziwa kwa ajii ya kusindika, kuuza kwenye hoteli na vioski. (Makofi)