Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 13 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 217 2024-02-15

Name

Agnes Elias Hokororo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. AGNES E. HOKORORO aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani kwa watumishi wanaokaimu nafasi kwa muda mrefu katika Vyuo vya FETA ikiwemo Mtwara?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibuĀ¬: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Agnes Elias Hokororo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kutokana na changamoto za kimuundo (organization structure) ya Wakala ya Elimu na Mafunzo ya Uvuvi (Fisheries Education and Training Agency - FETA) watumishi wengi waliokuwa wanakaimu kwa muda mrefu walishindwa kuthibitishwa katika nafasi zao. Changamoto hiyo ya kimuundo imeisha baada ya Muundo mpya wa FETA kuidhinishwa mwezi Oktoba, 2022.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa Serikali inaendelea na taratibu za kujaza nafasi za uongozi katika Muundo huo mpya ikiwemo kuwafanyia upekuzi wote wanaokaimu ili wakikidhi vigezo wathibitishwe katika nafasi hizo au kama hawakidhi vigezo wateuliwe watumishi wengine kujaza nafasi hizo.