Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 14 Sitting 13 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 221 2024-02-15

Name

Yustina Arcadius Rahhi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. YUSTINA A. RAHHI aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji katika Skimu ya Dongobeshi kufuatia kukamilika ujenzi wa Bwawa la Dongobeshi?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante sana na kwa niaba ya Waziri wa kilimo, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Yustina Arcadius Rahhi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea na upembuzi yakinifu na usanifu wa kina katika Skimu ya Dongobeshi kupitia mshauri elekezi ambaye anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo mwezi Mei, 2024.

Mheshimiwa Spika, kukamilika kwa kazi za upembuzi yakinifu na usanifu inayotekelezwa na mshauri elekezi, itawezesha kupatikana kwa gharama halisi zinazohitajika kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji. Kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji katika skimu hiyo kutanufaisha zaidi ya wakulima 1,300 katika Kata ya Dongobeshi.