Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Yustina Arcadius Rahhi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. YUSTINA A. RAHHI aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji katika Skimu ya Dongobeshi kufuatia kukamilika ujenzi wa Bwawa la Dongobeshi?

Supplementary Question 1

MHE. YUSTINA A. RAHHI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Nami nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, kwa kuwa Serikali imeshawekeza gharama kubwa kwenye Skimu ya Dongobeshi shilingi bilioni 2.5 kwa maana ya kukalimisha tuta na torosho la maji. Je, Serikali haioni sasa ni wakati wa kuweka kipaumble kukamilisha miundombinu iliyobaki kwa maana ya banio, vitorosha maji pamoja na kusakafia mifereji mikubwa?

Mheshimiwa Spika, swali langu la pili; Serikali inawekeza gharama kubwa sana kujenga miundombinu ya umwagiliaji, lakini haitoi mafunzo kwa wakulima pamoja na viongozi wa Tume ya Maji. Je, kwa ajili ya kudumisha uendelevu wa miradi ya umwagiliaji, Serikali sasa haioni umuhimu wa kuwapa mafunzo viongozi wa Tume ya Maji kabla na baada tu ya kuimarisha miradi ya umwagiliaji? Ahsante.

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana, jambo moja ni kwamba, ndiyo maana atakapomaliza kazi Mshauri Mwelekezi Mwezi Mei ni kwamba kitakachofuata baada ya hapo ni kuweka huu mradi kwa ajili ya mwaka wa fedha unaokuja ili uanze kujengwa. Kwa hiyo, ni sehemu ya vipaumbele vyetu sisi kama Wizara kuhakikisha Mradi wa Dongobeshi katika mwaka wa fedha ujao unaanza kutekelezwa. Kwa hiyo, lipo katika kipaumbele chetu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu mafunzo, tunafanya hivyo kwa sababu katika kila mradi tunaweka bajeti kwamba, baada ya mradi kukamilika, wale watumiaji wa maji kwa maana mradi mzima lazima wapatiwe mafunzo ya namna bora ya kutumia, na vilevile, kuutunza ule mradi husika. Kwa hiyo, jambo hilo lipo na kikubwa tu tutaongeza kasi ili tuweze kuwafikia watu wengi, ahsante sana.

Name

Dr. Florence George Samizi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Muhambwe

Primary Question

MHE. YUSTINA A. RAHHI aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji katika Skimu ya Dongobeshi kufuatia kukamilika ujenzi wa Bwawa la Dongobeshi?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. FLORENCE G. SAMIZI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza swali la nyongeza.

Je, ni lini Serikali itakarabati Skimu za Umwagiliaji za Nyendara, Muhambwe, Kumbanga na Kugorogondo katika Jimbo la Muhambwe?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nimthibitishie tu Mheshimiwa Mbunge kwamba moja ya wajibu mkubwa wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ambayo inafanya kazi sasa hivi, ni kufanya upembuzi yakinifu na ufafanuzi wa kina kwa miradi yote ya umwagiliaji, maana yake, malengo tuliyonayo sasa hivi ni kujenga mabwawa pamoja na schemes zikiwemo hizi ambazo Mheshimiwa Mbunge amezitaja za Garara, Muhambwe na miradi mingine ambayo ameitaja hapa. Kwa hiyo, tuko katika kazi na tukishamaliza hapo, maana yake tutatenga fedha katika bajeti yetu ili tuanze kuzijenga na nyingine kuzikarabati, ahsante.

Name

Shabani Omari Shekilindi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lushoto

Primary Question

MHE. YUSTINA A. RAHHI aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa miundombinu ya Umwagiliaji katika Skimu ya Dongobeshi kufuatia kukamilika ujenzi wa Bwawa la Dongobeshi?

Supplementary Question 3

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika, kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha na kupelekea udongo wenye rutuba kwenda mabondeni, je, Serikali haioni kuwa kuna haja ya kujenga mabwawa katika Kata ya Makanya, Gare, Kwayi pamoja na maeneo mengine katika Jimbo la Lushoto?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI K.n.y. WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Mpango wa Serikali ni kujenga Mabwawa katika maeneo yote ambayo tunaweza tukakusanya maji yakatumika katika kipindi chote cha mwaka ili Watanzania waweze kuingia katika kilimo kinachotumia maji badala ya kutegemea msimu mmoja wa mvua.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, mpango wetu ni pamoja na kutumia ikiwemo Bonde la Makanya, lipo katika mpango. Ndiyo maana mwaka huu wa 2022/2023 tuliomba Serikali itupitishie bajeti kwa ajili ya ujenzi wa mabwawa 100. Kwa hiyo, hilo ndilo lengo la Serikali na tutafanya hivyo. Ahsante sana.