Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 3 Industries and Trade Wizara ya Viwanda na Biashara 36 2024-04-04

Name

Mwanaisha Ng'anzi Ulenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza:-

Je, kuna mkakati gani wa kufufua viwanda vilivyokufa katika Mkoa wa Tanga?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea na mikakati mbalimbali ya kufufua viwanda vilivyokufa ukiwemo Mkoa wa Tanga, kwa kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wamiliki wa viwanda vilivyobinafsishwa, wenye nia ya kuviendeleza, kuvirejesha Serikalini na kuvitangaza upya kwa njia ya zabuni ya wazi; viwanda vilivyobinafsishwa kwa wamiliki walioshindwa kuviendeleza kabisa; na pia kuendelea kuvutia wawekezaji wapya wa kujenga viwanda vipya kwa kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini. Nakushukuru.