Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 52 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 460 | 2022-06-27 |
Name
Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muleba kusini
Primary Question
MHE. DKT.OSCAR I. KIKOYO aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itajenga Chuo cha VETA katika Wilaya ya Muleba?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba sasa kujibu swali la Dkt. Ishengoma Kikoyo, Mbunge wa Muleba Kusini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kujenga Vyuo vya VETA katika Mikoa na Wilaya mbalimbali kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha.
Mheshimiwa Spika, katika kipindi ambacho Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA katika Wilaya ya Muleba na maeneo mengine, wananchi wa Muleba wanashauriwa kuendelea kutumia Kituo cha Ufundi Stadi katika Wilaya ya Muleba kinachoitwa Ndolage VTC pamoja na vyuo vya VETA na Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi vilivyopo kwa ajili ya kupata elimu na mafunzo ya ufundi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved