Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 7 Sitting 52 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 461 2022-06-27

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kukarabati Chuo Kikuu cha Dodoma na Vyuo vingine ambavyo vilijengwa na kuonekana vina dosari?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Thea Medard Ntara, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Vyuo Vikuu nchini huanzishwa kwa kuzingatia taratibu na miongozo maalum inayotambulika na Sheria ya Vyuo Vikuu nchini.

Mheshimiwa Spika, kupitia utekelezaji wa Mradi wa Higher Education for Economic Transformation (HEET), Serikali itaboresha miundombinu kwa kujenga na kukarabati Taasisi 23 za Elimu ya Juu ikiwemo Vyuo Vikuu vya Umma ambapo Chuo Kikuu cha Dodoma ni miongoni mwa vyuo hivyo.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.