Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kukarabati Chuo Kikuu cha Dodoma na Vyuo vingine ambavyo vilijengwa na kuonekana vina dosari?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu ya Naibu Waziri yanayoonesha angalau matumaini, nina swali moja la nyongeza. Je, atatuhakikishia kwamba ukarabati utaendana sambamba na kuweka vifaa vya ufundishaji katika vyuo vyote ikiwemo vyuo vya kati? (Makofi)

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Ntara, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyozungumza kwenye jibu la msingi kwamba, tumepata mkopo wa zaidi ya dollar milioni 425, matumizi makubwa ya mkopo huu ni kuhakikisha tunakwenda kuviongezea miundombinu vyuo vyetu hivi vikuu, lakini vilevile tunakwenda kuboresha mitaala na kuanzisha mitaala mipya na vilevile tunakwenda kusomesha Walimu/Wahadhiri kwa ajili ya vyuo hivi. Sambamba na hivyo tunakwenda kununua vifaa kwa ajili ya vyuo vikuu vyote vya umma nchini. Kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi hili eneo la vifaa nalo vilevile limezingatiwa. Kwa vile amezungumzia vilevile vyuo vya kati, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge vyuo vya kati navyo tumevitengenezea mkakati wake maalum kabisa.

Mheshimiwa Spika, kwanza tuna mradi wetu wa EASTRIP ambao zaidi ya Dollar za Kimarekani milioni 75 tumeweza kusaini kwa ajili ya ujenzi wa vyuo hivyo lakini vilevile kwa ajili ya ununuzi wa vifaa. Kwa hiyo, sambamba na huu mradi wetu wa HEET ambao utashughulikia vyuo vikuu, lakini tuna miradi mingine midogo midogo ambayo itashughulikia vyuo hivi vya kati kwa kuhakikisha kunakuwa na wahadhiri wa kutosha na vifaa vya kujifunzia na kufundishia kwenye vyuo vyetu.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.

Name

Maryam Azan Mwinyi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Chake Chake

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kukarabati Chuo Kikuu cha Dodoma na Vyuo vingine ambavyo vilijengwa na kuonekana vina dosari?

Supplementary Question 2

MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Kwa vile Serikali ina mpango wa ukarabati wa vyuo vikuu hapa nchini. Je, Serikali ina mpango gani wa kukarabati vyuo vikuu vilivyopo kule Zanzibar? (Makofi)

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Maryam Mwinyi, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza kwenye majibu yangu ya msingi kwamba, mkopo huu wetu wa HEET (Higher Education for Economic Transformation) unakwenda kuboresha maeneo yote ya vyuo vikuu vya umma vikiwemo na vile vya Zanzibar. Kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi chuo chetu kile cha SUZA Zanzibar kimepata gawio katika gawio hili la mradi wetu wa HEET lakini taasisi yetu ile ya Marine Science ya Zanzibar ambayo inasimamiwa na Chuo chetu cha Dar es Salaam nayo vilevile sio tu inakwenda kuboreshwa bali inakwenda kujengwa upya. Kwa hiyo, nimwondoe wasiwasi Zanzibar nayo tumeizingatia kwenye mgao huu na tutahakikisha kwamba kazi hii inakwenda kufanyika kwa haraka.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.

Name

Dr. Paulina Daniel Nahato

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kukarabati Chuo Kikuu cha Dodoma na Vyuo vingine ambavyo vilijengwa na kuonekana vina dosari?

Supplementary Question 3

MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Mheshimiwa Waziri Chuo Kikuu cha Muhimbili majengo yake ni chakavu eneo ni dogo wanafunzi ni wengi kila mwaka. Je, Serikali inatoa kauli gani kuitanua Chuo Kikuu cha Madaktari Muhimbili ili kiweze kukidhi haja ya kututolea madaktari wengi nchini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante.

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Dkt. Nahato, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwanza tukiri kwamba Chuo chetu cha Muhimbili eneo lake limebana sana, lakini sisi Serikali tayari tumeshaliona hilo na kwa kutambua hilo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika mradi wetu huu wa HEET tunakwenda kufanya mageuzi makubwa sana katika Chuo chetu hiki cha Muhimbili kwa kujenga campus au chuo kingine kipya kabisa katika eneo letu la Mloganzila ambalo litakuwa na fani au ndaki tofauti tofauti.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo haikutosha, tunakwenda tena kufungua campus nyingine mpya katika Mkoa wa Kigoma ambayo itasimamiwa na Muhimbili. Hiyo vilevile haitoshi, tena tunakwenda kufanya hivyo katika Mkoa wa Mbeya kwa kujenga campus nyingine hii ya Muhimbili. Kwa hiyo, mchakato huu umeshaanza, nimwondoe wasiwasi tutadahili pale wanafunzi wa kutosha kuhakikisha kwamba tunapata wataalam wa tiba hapa hapa nchini. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.

Name

Bakar Hamad Bakar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

House of Representatives

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kukarabati Chuo Kikuu cha Dodoma na Vyuo vingine ambavyo vilijengwa na kuonekana vina dosari?

Supplementary Question 4

MHE. BAKAR HAMAD BAKAR: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa, elimu ya juu ni sekta ya Muungano na kwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Mwinyi ameitangaza Pemba kwamba ni eneo maalum la uwekezaji. Je, ni upi mpango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kupitia Wizara hii wa kuwekeza kwenye sekta hii ya elimu kwa kujenga Chuo Kikuu Pemba? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ahsante.

Name

Gibson Blasius Meiseyeki

Sex

Male

Party

CHADEMA

Constituent

Arumeru-Magharibi

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali dogo la nyongeza la Mheshimiwa Bakar Bakar, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli anachozungumza Mheshimiwa Mbunge kwamba Wizara hii ni Wizara ya Muungano hasa hasa kwenye masuala ya elimu ya juu, lakini kama nilivyokwishaeleza katika maswali yaliyopita, katika mradi wetu wa HEET tunakwenda kufanya ujenzi mkubwa katika eneo lile la Zanzibar kwa upande wa Chuo chetu kile cha Marine Institute ambapo nacho vilevile kitatengeneza branch baadaye katika Kisiwa cha Pemba.

Mheshimiwa Spika, naomba nimwondoe wasiwasi kwa kadri muda utakavyokwenda, tutaifikia Pemba. Hivi sasa mkakati uliopo vilevile chuo chetu cha masafa marefu, hiki Chuo Kikuu Huria tayari kina branch pale Pemba na katika mgao huu kimenufaika na maeneo ambayo yanakwenda kuboreshwa ni pamoja na tawi letu lile la Chuo Kikuu Huria pale katika Kisiwa cha Pemba ambacho nacho vilevile ni chuo kikuu kwa mujibu wa sheria.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.