Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 43 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 555 2024-06-07

Name

Seif Khamis Said Gulamali

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manonga

Primary Question

MHE. DENNIS L. LONDO K.n.y. MHE. SEIF K. S. GULAMALI aliuliza:-

Je, Serikali itawaunga mkono World Vision kuendeleza ujenzi wa Chuo cha VETA Choma?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua juhudi za wadau mbalimbali katika kuongeza fursa za upatikanaji wa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi nchini ikiwemo Word Vision ambao pamoja na juhudi zingine wanendelea na ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kinachojengwa katika Wilaya ya Igunga. Aidha, Serikali inaendelea na azma yake ya kuhakikisha kila Wilaya nchini inakuwa na Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali imekamilisha ujenzi wa Vyuo 25 vya VETA vya Wilaya pamoja na vyuo vinne vya VETA vya Mikoa ambapo Wilaya ya Igunga ambayo World Vision inaendelea na ujenzi wa Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi ni miongoni mwa Wilaya zilizojengewa vyuo hivi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ipo tayari kuunga mkono juhudi hizo na imeshaelekeza Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) kutembelea chuo hicho na kuwasilisha maeneo yanayopendekezwa Serikali iunge mkono ili chuo hiki kiweze kukamilika na kuanza kutoa mafunzo kama ilivyopangwa. Nakushukuru. (Makofi)