Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 14 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 178 2024-04-25

Name

Husna Juma Sekiboko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza:-

Je, Serikali haioni haja ya mikopo ya 10% inayotolewa na halmashauri kutolewa kwa mjasiriamali mmoja mmoja?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, mikopo ya 10% inatolewa kwa mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura 290, Kifungu cha 37A. Kifungu hicho kimeeleza namna halmashauri zote zinavyopaswa kutenga 10% ya mapato yake ya ndani kwa ajili ya mikopo isiyo na riba kwa vikundi vilivyosajiliwa vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Mheshimiwa Spika, Serikali itaufanyia tathmini utaratibu wa mikopo ya 10% kutolewa kwa mjasiriamali mmoja mmoja ili kuona tija na ufanisi wake ili ikibidi maboresho yafanyike. Ahsante.