Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 14 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 179 2024-04-25

Name

Boniphace Nyangindu Butondo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kishapu

Primary Question

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza:-

Je, lini Kituo cha Afya cha Nhobola kitafanyiwa ukarabati baada ya kuwa chakavu kwa kipindi kirefu ikiwa ni pamoja na upanuzi wa kituo hiki?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Nhobola ni miongoni mwa Vituo vya Afya 202 kongwe ambavyo vinahitaji ukarabati mkubwa ili kuendana na mahitaji ya sasa ya utoaji wa huduma za afya.

Mheshimiwa Spika, Serikali itavifanyia ukarabati vituo hivyo kwa awamu kikiwemo Kituo cha Afya Nhobola katika Halmashauri ya Kishapu, ahsante.