Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 14 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 186 | 2024-04-25 |
Name
Maimuna Ahmad Pathan
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza:-
Je, kuna mpango gani wa kukarabati Mabwawa ya Naipingo, Chemchem, Mkumba, Farm Four na Eight, Ntila na JKT Nachingwea?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea kubaini na kufanya ukarabati na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya umwagiliaji yakiwemo mabwawa na skimu za umwagiliaji nchini. Kipaumbele kimeelekezwa katika maeneo makubwa yanayohusisha wakulima wengi na kwa yale yanayohusisha wakulima wachache. Serikali imejikita zaidi kuendeleza kwa kuchimba visima ambapo kisima kimoja kinaweza kuhudumia ekari 40.
Mheshimiwa Spika, maeneo yaliyotajwa na Mheshimiwa Mbunge ni miongoni mwa maeneo yenye hekta chache ambapo Serikali kwa mwaka wa fedha 2023/2024 imepanga kuchimba visima katika Skimu ya Ntila. Aidha, kwa Mabwawa ya Naipingo, Nkumba, Chemchem, Farm Four na Eight, Tume ya Taifa ya Umwagiliaji itaendelea kuyabaini kwa kushirikiana na Ofisi ya Mbunge na Halmashauri ili nayo yafikiwe kadri bajeti itakavyoruhusu.
Mheshimiwa Spika, Bwawa la JKT Nachingwea ni miongoni mwa mabwawa yaliyopo chini ya Jeshi la Kujenga Taifa ambalo ndilo linaloratibu uendelezaji na usimamizi wake. Hivyo, nitawasiliana na Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ili kulikarabati bwawa hilo, chini ya uratibu wake.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved