Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Maimuna Ahmad Pathan

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MAIMUNA A. PATHAN aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kukarabati Mabwawa ya Naipingo, Chemchem, Mkumba, Farm Four na Eight, Ntila na JKT Nachingwea?

Supplementary Question 1

MHE. MAIMUNA A. PATHAN: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; kutokana na majibu ya Waziri amesema kwamba, Kisima cha Ntila kitaanza kuchimbwa mwaka huu wa fedha na najua imebaki miezi miwili tu. Je, ni lini hasa kisima hiki kitachimbwa au kimeshachimbwa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kutokana na majibu ya swali la msingi. Je, Waziri yuko tayari sasa kuongozana na Mheshimiwa Mbunge wangu wa jimbo hilo ili aende akabaini maeneo haya kulingana na majibu aliyojibu?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ni kweli, kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha unaoisha Juni, imebaki miezi miwili na kwamba, hatua iliyopo sasa hivi ni kwamba, tunatafuta mkandarasi kwa ajili ya kuchimba, maana yake tenda ilikuwa imetangazwa. Kwa hiyo, tukishamaliza maana yake tutasaini mkataba na kazi itaendelea, kikubwa tu ni kwamba, kazi lazima ianze katika mwaka huu wa fedha..

Mheshimiwa Spika, kuhusu utayari wa mimi kufika; niko tayari kuongozana na Mheshimiwa Mbunge pamoja na Mheshimiwa Mbunge wa Viti Maalum kwenda kujionea kazi nzuri ambayo imefanywa huko na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, lakini na kujionea changamoto chache ambazo zinahitaji ufumbuzi. Kwa hiyo, niko tayari, ahsante sana.