Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 43 | Information, Communication and Information Technology | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 560 | 2024-06-07 |
Name
Joseph Michael Mkundi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukerewe
Primary Question
MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itaongeza nguvu ya mnara katika Kata ya Bukiko kutoka 2G hadi 3G na kuweka generator kwa kuwa kata hiyo ina shida kubwa ya mawasiliano?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) itaijumuisha kata ya Bukiko katika mradi wa kuboresha huduma za mawasiliano kwa kuongeza teknolojia za 3G na 4G na pia mradi huu utaimarisha miundombinu ya nishati ikiwemo ya kuweka generator. Utekelezaji wa mradi huu utaanza katika mwaka wa fedha wa 2024/2025.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved