Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Joseph Michael Mkundi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukerewe
Primary Question
MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaongeza nguvu ya mnara katika Kata ya Bukiko kutoka 2G hadi 3G na kuweka generator kwa kuwa kata hiyo ina shida kubwa ya mawasiliano?
Supplementary Question 1
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali na nina maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kuwa bajeti ya kazi hii ilitengwa kwenye mwaka wa fedha 2022/2023 lakini utekelezaji wake umekuwa unasogezwa mbele kila wakati, Serikali haiona kwamba inakwamisha maendeleo ya wananchi wa Kata hii ya Bukiko?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa changamoto za mawasiliano kwenye Jimbo la Ukerewe zipo maeneo mengi, Mheshimiwa Naibu Waziri upo tayari kufanya ziara Jimboni Ukerewe ili upate uhalisia wa changamoto hizi na kupata ufumbuzi wa kitaalamu wa uhakika kwa ajili ya matatizo haya? Nashukuru.
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Joseph Mkundi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kukamilisha maendeleo naomba nimtoe hofu Mheshimiwa Mbunge pamoja na wananchi wote wa Ukerewe, Serikali haiwezi kukwamisha maendeleo, imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kupitia mnara uliopo na naomba nikupe uhakika kazi hii inakwenda kuimarishwa mwaka ujao wa fedha na tutaisimamia pamoja mimi na wewe.
Mheshimiwa Naibu Spika, suala la kufanya ziara Mheshimiwa Mbunge ni wajibu wangu, hakuna shida baada ya hapa tuonane tuweze kupanga ratiba ya pamoja.
Name
Prof. Patrick Alois Ndakidemi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Vijijini
Primary Question
MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaongeza nguvu ya mnara katika Kata ya Bukiko kutoka 2G hadi 3G na kuweka generator kwa kuwa kata hiyo ina shida kubwa ya mawasiliano?
Supplementary Question 2
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi.
Mheshimiwa Naibu Spika, Kampuni ya Simu ya Tigo ilishinda zabuni ya kutengeneza mnara wa mawasiliano ya simu katika Kata ya Uru Shimbwe, lakini kazi hii ni kama vile haijaanza; je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba inasimamia utekelezaji wa mradi huu?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ndakidemi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze amekuwa akifuatilia hili na nitoe tu wito kwa makampuni yote ambayo yamepewa kazi, tunahitaji kuona kazi zinafanyika kwa wakati na nitasimamia hili mimi mwenyewe Mheshimiwa Mbunge usipate shaka.
Name
Asia Abdulkarim Halamga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaongeza nguvu ya mnara katika Kata ya Bukiko kutoka 2G hadi 3G na kuweka generator kwa kuwa kata hiyo ina shida kubwa ya mawasiliano?
Supplementary Question 3
MHE. ASIA A. HALAMGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali.
Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wa Kata ya Gehandu kwa sasa wanatumia mnara wa mawasiliano uliopo Kata ya Ishiponga. Je, ni lini Serikali itapeleka mnara wa mawasiliano katika Kata ya Gehandu kwa sababu huu wa Ishiponga katika Jimbo la Hanang unasuasua? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Asia Halamga na nimpongeze sana Mheshimiwa Mbunge kwa ufuatiliaji wake.
Mheshimiwa Naibu Spika, hili eneo la Gehandu tayari tunalifanyia kazi, kwanza, kuboresha ule mnara wa jirani kwa sababu masuala ya mawasiliano ni suala la signals kufika. Kwa hiyo, tutaongezea vifaa ili kuona signals zinaweza kufika vizuri zaidi wakati tunajipanga kujenga mnara mpya katika eneo hili la Gehandu. (Makofi)
Name
Sophia Hebron Mwakagenda
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaongeza nguvu ya mnara katika Kata ya Bukiko kutoka 2G hadi 3G na kuweka generator kwa kuwa kata hiyo ina shida kubwa ya mawasiliano?
Supplementary Question 4
MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika Kata ya Ilima, Jimbo la Rungwe, Kijiji cha Katundulu kuna shida kubwa sana ya usikivu wa minara ya simu; ni lini Serikali mtatuletea mnara katika kijiji kile? (Makofi)
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Sophia Mwakagenda, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, hili eneo la Ilima tayari lipo katika mpango wa Wizara. Napenda kukutoa hofu tunakwenda kujenga mnara, lakini vilevile kuhakikisha tunaongezea vifaa katika minara ya jirani ili signals ziweze kufika Ilima na maeneo yote yale ya jirani. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved