Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 43 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 562 | 2024-06-07 |
Name
Francis Kumba Ndulane
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Primary Question
MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza: -
Je, lini Serikali itawapatia mbegu bora za ufuta wananchi wa Wilaya ya Kilwa waweze kuzalisha ufuta mwingi kwani wanatumia mbegu za asili?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuwahamasisha wakulima wa zao la ufuta katika Wilaya ya Kilwa kutumia mbegu bora ili kuongeza uzalishaji. Katika msimu wa mwaka 2023/2024 Serikali ilisambaza bure jumla ya tani 10 za mbegu bora ya ufuta kwa wakulima wa Kilwa na kuweka mashamba ya mfano ya kilimo bora cha ufuta katika Kata za Likawage na Mandawa. Aidha, Serikali kupitia Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) imetoa elimu kwa wakulima katika Kata za Miguruwe na Mandawa kuhusu umuhimu wa matumizi ya mbegu bora na kanuni za kilimo bora cha zao la ufuta ili kuongeza tija. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved