Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Francis Kumba Ndulane
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilwa Kaskazini
Primary Question
MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza: - Je, lini Serikali itawapatia mbegu bora za ufuta wananchi wa Wilaya ya Kilwa waweze kuzalisha ufuta mwingi kwani wanatumia mbegu za asili?
Supplementary Question 1
MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, zao hili la ufuta katika Wilaya ya Kilwa limekuwa likikabiliwa sana na changamoto ya wadudu waharibifu pamoja na kukosa dawa; je, Serikali ina mkakati gani wa kukakikisha kwamba inapeleka dawa za kuua wadudu katika zao hili? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kufuatia kuwepo kwa mvua kubwa za El–Nino na Kimbunga Hidaya, mazao ya minazi na michungwa yapatayo 100,000 yamezolewa na mafuriko; je, Serikali ina mkakati gani wa kusaidia wakulima wa mazao haya ya minazi na michungwa ili kuhakikisha kwamba tunarudisha mazao haya katika uzalishaji wa kawaida? (Makofi)
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana na nimpongeze Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini kwa kuendelea kuwafuatilia kwa karibu wananchi wake hususani wanaoji-engage katika kilimo.
Mheshimiwa Naibu Spika, jambo moja namthibitishia tu kwamba panapotokea uharibifu wowote, moja ya jukumu letu sisi kama Wizara ni kuleta dawa ama viuatilifu kwa ajili ya kuondoa hiyo changamoto ya mazao ambayo itakuwa imewapata. Kwa hiyo, tunachohitaji tu ni kupewa taarifa kutoka katika halmashauri husika ama mkoa husika na sisi tutafanya kazi hiyo. Kwa hiyo, tuko tayari muda wowote kutekeleza jambo hilo. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu minazi ambayo imechukuliwa, nakuthibitishia tu kwamba kabla ya mwezi wa kumi mwaka huu Wizara tutasambaza minazi bure kwa wananchi ambao walikutwa na adha hiyo, ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved