Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 45 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 584 | 2024-06-11 |
Name
Abubakar Damian Asenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilombero
Primary Question
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA aliuliza: -
Je, lini Serikali itajenga Chuo cha Ufundi VETA katika Mji wa Ifakara?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kwa sasa inaendelea na utekelezaji wa azma ya kujenga Chuo cha Ufundi Stadi katika kila mkoa na wilaya nchini. Katika mwaka wa fedha 2022/2023 Serikali ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kujenga Vyuo vya Ufundi Stadi katika wilaya 64 ambazo zilikuwa hazijajengewa Vyuo vya Ufundi Stadi pamoja na Chuo cha Mkoa wa Songwe. Aidha, Wilaya ya Kilombero ni miongoni mwa wilaya 64 ambazo zinajengewa vyuo vya ufundi stadi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa Serikali imeshapeeka kiasi cha shilingi 324,694,243 pamoja na vifaa vya ujenzi ikiwemo nondo na simenti kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Kilombero ambacho kitatoa mafunzo kwa vijana wa Wilaya ya Kilombero ikiwemo Mji wa Ifakara. Aidha, ujenzi wa chuo hiki upo katika hatua ya ujenzi wa kuta za boma na ufungaji wa linta pamoja na ukamilishaji wa misingi, nakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved