Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 15 Sitting 18 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 230 2024-05-03

Name

Jonas William Mbunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Mjini

Primary Question

MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Barabara ya Mbinga Mpepai hadi Mtua kwa kiwango cha changarawe?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ya Mbinga Mpepai – Mtua ambayo inatambulika kwa jina la Mbinga – Liparamba yenye urefu wa kilometa 41.87 ipo kwenye utekelezaji kwa mwaka huu wa fedha 2023/2024, na wakandarasi wapo eneo la kazi. Serikali kupitia TARURA imetenga shilingi milioni 947.2 ambazo zitatumika kutengeneza kilometa 31 kwa kiwango cha changarawe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mradi wa TACTIC itatekeleza ujenzi wa barabara hii kilomita mbili kwa kiwango cha tabaka la lami. Serikali itaendelea kuhudumia mtandao wa barabara katika Mji wa Mbinga ikiwemo barabara hii kulingana na upatikanaji wa fedha.