Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 18 | Lands, Housing and Human Settlement Development | Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi | 240 | 2024-05-03 |
Name
Jafari Chege Wambura
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Rorya
Primary Question
MHE. JAFARI W. CHEGE aliuliza: -
Je, lini Serikali itahamisha Mabaraza ya Ardhi kwenda kwenye Mfumo wa Mahakama?
Name
Jerry William Silaa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukonga
Answer
WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Jafari Wambura Chege, Mbunge wa Rorya, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika jitihada za kuboresha mfumo uliopo wa utatuzi wa migogoro ya ardhi nchini, Serikali kupitia Wizara ya Katiba na Sheria imeandaa mapendekezo ya kuhamisha shughuli zinazofanywa na Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwenda katika mhimili wa Mahakama. Pindi taratibu zitakapokamilika, Serikali italifahamisha Bunge lako Tukufu, nakushukuru. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved