Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 19 | Good Governance | Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) | 245 | 2024-05-06 |
Name
Vita Rashid Kawawa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Namtumbo
Primary Question
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI K.n.y. MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza: -
Je, ni kwa nini wanufaika wa TASAF wanalazimika kufuata fedha benki hata fedha hiyo ikiwa ni kidogo?
Name
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chalinze
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu wa malipo kwa wanufaika wa TASAF unafanyika kwa njia kuu tatu: kwanza, kupitia akaunti ya Benki; pili, kupitia akaunti ya simu ya mkononi; na tatu, kwa malipo taslimu kupitia kwa wakala au katika kituo cha malipo. Uamuzi wa njia gani ambayo mlengwa atapenda kulipwa, unabaki kuwa wa kwake mwenyewe mlengwa ambaye anatambulika wakati wa uandikishaji wa daftari la walengwa.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved