Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Charles Stephen Kimei
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vunjo
Primary Question
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI K.n.y. MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza: - Je, ni kwa nini wanufaika wa TASAF wanalazimika kufuata fedha benki hata fedha hiyo ikiwa ni kidogo?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, naomba niulize swali la nyongeza. Kwa kuwa ile database ya watu ambao wanastahili kupata fedha za TASAF, iliboreshwa, je, Serikali imefikia hatua gani ya kuchakata takwimu za Sensa ya 2022 ili kuweza kujua ni wahitaji gani? (Makofi)
Name
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chalinze
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea na uchakataji wa taarifa za takwimu halisia juu ya mahitaji ya Watanzania wangapi ambao wanatakiwa waangaliwe katika awamu ijayo ya TASAF. Kwa hiyo, nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba tutakapokuwa tumekamilisha hatua hizo, tutawajulisha kupitia vile vikao vyetu maalumu vya TASAF katika ngazi yetu ya vijiji.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, katika kila sehemu ambayo watu watakuwa wanatakiwa kuingia kwenye daftari jipya la TASAF, basi nafasi itatolewa ili Watanzania waweze kupata fursa hiyo ya kuendelea kusaidiwa katika hatua za kupunguza umasikini.
Name
Anatropia Lwehikila Theonest
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHARLES S. KIMEI K.n.y. MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza: - Je, ni kwa nini wanufaika wa TASAF wanalazimika kufuata fedha benki hata fedha hiyo ikiwa ni kidogo?
Supplementary Question 2
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Wakati mwingine wanufaika wa TASAF huondolewa kwenye mfumo pengine kwa kutokuelewa vigezo au kwa kuonewa. Ni kwa nini vigezo haviko dhahiri ili pale mnufaika anapoondolewa kwenye TASAF kusiwepo na malalamiko ya kuonekana kwamba wanaondolewa kwa sababu za kisiasa? (Makofi)
Name
Ridhiwani Jakaya Kikwete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chalinze
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, kwa mujibu wa taratibu za TASAF, katika Mkutano Mkuu wa Kijiji, Shehia au Mtaa ambapo majina ya wanufaika ndipo yanatakiwa kusemwa, pale hatua ya kwanza inapofanyika ni kueleza sifa gani ambazo mtu anatakiwa kuwa nazo ili aingie kwenye Mfuko wa TASAF.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, kama inatokea mtu hajasikia zile sifa au mtu ambaye hana zile zifa na ameingizwa kwenye TASAF, utaratibu wa ukataji wa rufaa kwa mwananchi ambaye hajaridhishwa na uingizaji huo, zinatakiwa zifuatwe.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kipo kikao cha uchujaji wa wale watu walioingizwa kwenye Mfuko wa TASAF. Kwa hiyo, siyo rahisi sana Mheshimiwa Mbunge kwa mtu ambaye hana sifa za kuwa ndani ya Mfuko wa TASAF kuwepo.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hata kama kule chini labda wanaoneana aibu na wanashindwa kumtoa mtu fulani, nafasi kwa ajili ya kukata rufaa mpaka kwenye ngazi ya Taifa nazo zinatakiwa zifuatwe ili wale wanaoratibu katika ngazi ya Taifa waweze kushuka mpaka kwenye ngazi ya Kijiji kwa ajili ya kwenda kutafuta ushahidi wa kujiridhisha juu ya huyo mtu aliyeingizwa katika mradi huo kimakosa au kinyume cha utaratibu.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved