Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 19 | Community Development, Gender and Children | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 255 | 2024-05-06 |
Name
Abeid Ighondo Ramadhani
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Singida Kaskazini
Primary Question
MHE. ABEID R. IGHONDO aliuliza:-
Je, Serikali ina mkakati gani wa kukomesha mapenzi ya jinsia moja nchini pamoja na ukatili dhidi ya watoto?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara yangu kwa kushirikiana na Wizara za kisekta inaratibu utekelezaji wa mikakati ya kukabiliana na tatizo la mmomonyoko wa maadili na ukatili dhidi ya watoto. Mikakati hiyo ni pamoja na:-
(i) Kusimamia utekelezaji wa Programu Jumuishi ya Taifa ya Malezi, Makuzi na Maendeleo ya Awali ya Mtoto pamoja na kuanzisha na kuimarisha madawati ya ulinzi na usalama wa mtoto katika shule za msingi, sekondari na vyuo; na
(ii) Kusimamia utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) pamoja na Mpango wa Taifa wa Kuwekeza katika Afya na Maendeleo ya Vijana Balehe (NAIHA). Aidha, Wizara itaendelea kutoa elimu kwa umma na kuongeza afua za malezi, makuzi na maendeleo ya mtoto pamoja na kuimarisha taasisi za familia kwa lengo la kupunguza au kumaliza kabisa changamoto ya mmomonyoko wa maadili nchini, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved