Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 9 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 143 | 2024-09-06 |
Name
Jackson Gedion Kiswaga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalenga
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA K.n.y. MHE. JACKSON G. KISWAGA aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa bwawa la umwagiliaji katika Kijiji cha Magubike Kata ya Nzihi – Kalenga?
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Jackson Kiswaga, Mbunge wa Kalenga, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetenga fedha kwa ajili ya kukamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Bwawa la Magubike pamoja na skimu kwa lengo la kuanza ujenzi katika mwaka wa fedha 2024/2025. Baada ya ujenzi huo kukamilika wananchi 1,200 watanufaika na kilimo cha umwagiliaji.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved