Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Justin Lazaro Nyamoga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilolo
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA K.n.y. MHE. JACKSON G. KISWAGA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa bwawa la umwagiliaji katika Kijiji cha Magubike Kata ya Nzihi – Kalenga?
Supplementary Question 1
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sababu mradi huu Mradi wa Magubike umechukua muda mrefu kidogo, je, Serikali haioni umuhimu wa kuharakisha ujenzi wa mradi huu ili wananchi wapate huduma?
Swali la pili, Mradi wa Umwagiliaji wa Mgambalenga ambao ujenzi wake umekuwa ukisuasua, je, Serikali inampango gani wakumwambia mkandarasi yule kuharakisha ujenzi kwa sababu tayari ana mkataba na analipwa. (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba mradi huu umekuwa wa muda mrefu lakini nataka niwahakikishie kwamba mwaka huu unatangazwa na mwaka huu utaanza kutekelezwa, lakini kuhusu Mgambalenga kulikuwa kuna matatizo ya kifedha nashukuru Wizara ya Fedha wameshatuandalia utaratibu wa kutupatia fedha, mkandarasi atarudi kuwa effective kufanya kazi yake. (Makofi)
Name
Samweli Xaday Hhayuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hanang'
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA K.n.y. MHE. JACKSON G. KISWAGA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa bwawa la umwagiliaji katika Kijiji cha Magubike Kata ya Nzihi – Kalenga?
Supplementary Question 2
MHE. SAMWELI X. HHAYUMA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza.
Je, Mheshimiwa Waziri, umeniahidi mara kadhaa kuhusu Mradi wa Bwawa la Ngindababiek, lini tutapata fedha ili mradi huo uweze kujengwa?
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumjibu Mheshimiwa Mbunge wa Hanang kama ifuatavyo; jana mimi na yeye tulikuwa pamoja, kaacha barua ofisini na nimeshatoa maelekezo. (Makofi)
Name
Prof. Patrick Alois Ndakidemi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Vijijini
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA K.n.y. MHE. JACKSON G. KISWAGA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa bwawa la umwagiliaji katika Kijiji cha Magubike Kata ya Nzihi – Kalenga?
Supplementary Question 3
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru, je, Serikali ina mkakati gani wa kuanza ujenzi wa Skimu ya Makeresho ambayo itakuwa msaada mkubwa sana kwa wakulima wa Kahawa katika Kata ya Kibosho Magharibi? (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kumjibu Profesa Ndakidemi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Makeresho tumeshaitangaza na sasa hivi ipo kwenye mfumo, tunasubiri mkandarasi apatikane In ShaaAllah mwaka huu wa fedha atakuwa site.
Name
Jonas Van Zeeland
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mvomero
Primary Question
MHE. JUSTIN L. NYAMOGA K.n.y. MHE. JACKSON G. KISWAGA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa bwawa la umwagiliaji katika Kijiji cha Magubike Kata ya Nzihi – Kalenga?
Supplementary Question 4
MHE. JONAS V. ZEELAND: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana, naomba kuuliza swali dogo la nyongeza.
Katika Kata ya Mkindo tuna mradi wa umwagiliaji wenye thamani ya shilingi bilioni 5.6, mkandarasi toka amepewa kazi mwaka juzi mpaka sasa hivi hajafika hata 50%. Je, lini atakamilisha ili mradi huu uweze kuwasaidia wakulima wetu wa Mkindo? (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimjibu Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli mkandarasi amekuwa akisuasua na amekuwa akitafuta sababu za kuhalalisha kuchelewesha utekelezaji wa mradi. Nataka tu nimhakikishie kuwa Wizara tumekuwa very close na yeye na si muda mrefu tuta-unlock matatizo yaliyopo kati ya sisi na yeye na ikishindikana tutatafuta njia sahihi ya kuachana ili hiyo ndoa ife, tutafute mkandarasi mwingine.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved