Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 16 Sitting 9 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Waziri wa Mifugo na Uvuvi 148 2024-09-06

Name

Joseph Zacharius Kamonga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ludewa

Primary Question

MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga vichanja na mahema ya kisasa ya kukaushia samaki na dagaa kwa kutumia nishati ya umeme na jua Ludewa?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kuboresha na kujenga miundombinu ya uvuvi katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mwambao wa Ziwa Nyasa. Miundombinu ya mahema na vichanja vya kukaushia samaki na dagaa husaidia kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi, kuongeza ubora, thamani na kuboresha biashara yake.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2024/2025 Serikali haina mpango wa kujenga vichanja na mahema ya kukaushia dagaa katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa. Aidha, Serikali inatekeleza mpango wa kupunguza upotevu wa mazao ya uvuvi na kuboresha biashara ya mazao hayo katika halmashauri hiyo ambapo imeanza ujenzi wa Soko la Samaki Manda katika Kijiji cha Nsungu, Kata ya Manda kuanzia mwaka wa fedha 2023/2024.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuzingatia umuhimu wa miundombinu hii, napenda kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa Wizara yangu itaendelea na jitihada za kuboresha miundombinu ya uvuvi kulingana na upatikanaji wa fedha. Aidha, ninaomba Halmashauri ya Ludewa itambue umuhimu ya miundombinu ya mahema na vichanja vya kukaushia samaki na dagaa na kuiweka kwenye miradi yake ya kimkakati kwa kutenga fedha kupitia mapato ya ndani.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)