Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Joseph Zacharius Kamonga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ludewa
Primary Question
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga vichanja na mahema ya kisasa ya kukaushia samaki na dagaa kwa kutumia nishati ya umeme na jua Ludewa?
Supplementary Question 1
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi na nimshukuru sana Mheshimiwa Rais kwa kutoa shilingi milioni 800 kwa ajili ya ujenzi wa soko la samaki pale Manda. Pamoja na hilo nina maswali mawili madogo ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa sasa Serikali imejenga soko hili la kisasa, je, ni lini Wizara itatuma wataalamu kwenda kutoa elimu ya ufugaji wa samaki kwa vizimba kwa wananchi? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, ni lini Serikali itakwenda kutoa elimu ya uhifadhi wa mazalia ya samaki kwa wananchi ili kuweza kuongeza idadi ya samaki kwenye Ziwa Nyasa? Ahsante.
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, tumepokea ombi la Mheshimiwa Mbunge na baada ya Bunge hili kuhitimishwa tutatuma wataalamu kwenda kutoa elimu ya vizimba ili wananchi wa eneo hilo waweze kupata elimu ya vizimba, lakini kwa taarifa tu ni kwamba baada ya mwezi wa tisa tayari utafiti wa namna gani vizimba vitakaa katika maeneo gani ya Ziwa Nyasa vitakuwa vimekamilika na wananchi wanaozunguka maeneo hayo wataruhusiwa sasa kuchukuwa vizimba kwa ajili ya kwenda kuweka katika Ziwa Nyasa.
Mheshimiwa Naibu Spika, hili la pili la kutoa elimu, Wizara imeendelea kutoa elimu kwa wavuvi katika maeneo mbalimbali nchini na hususani katika eneo la Mheshimiwa Mbunge kule Ludewa tutatuma wataalamu wataenda kutoa elimu na baada ya Bunge hili Tukufu tuwasiliane Mheshimiwa Mbunge tuone wavuvi gani wanahitaji elimu ili waweze kupatiwa elimu katika maeneo hayo, ahsante.
Name
Mwantumu Mzamili Zodo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga vichanja na mahema ya kisasa ya kukaushia samaki na dagaa kwa kutumia nishati ya umeme na jua Ludewa?
Supplementary Question 2
MHE. MWANTUMU M. ZODO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, je, ni lini Serikali itakwenda kujenga vichanja vya kuanikia samaki na dagaa kwa ukanda wetu wa Pwani hasa Pwani ya Tanga kwa maeneo ya Mkinga, Muheza, Tanga pamoja na Pangani kama ilivyotuahidi? (Makofi)
Name
Alexander Pastory Mnyeti
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Misungwi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama nilivyosema katika jibu la msingi kwamba kwa sasa Serikali haina mpango wa kujenga vichanja isipokuwa tunahamasisha halmashauri husika zijikite kwenye kuweka kwenye miradi wa mkakati kujenga vichanja hivyo kwa sababu ndiyo vinasidia watu hao, lakini pia halmashauri zinajipatia mapato kupitia vichanja hivyo, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved