Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 5 | Information, Communication and Information Technology | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 87 | 2024-09-02 |
Name
Juma Usonge Hamad
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chaani
Primary Question
MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. JUMA USONGE HAMAD aliuliza: -
Je, lini Serikali itatuma wataalamu kwenda Kijiji cha Kandwe kilichopo Wilaya ya Kaskazini Unguja ili kutatua changamoto ya mawasiliano?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) imeendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya kufikisha huduma za mawasiliano katika pande zote mbili za Muungano kwa kushirikiana na watoa huduma. Kwenye mradi wa kufikisha mawasiliano katika Shehia (Kata) 38 Visiwani Zanzibar uliokamilika mwaka 2022, Kijiji cha Kandwi kilijumuishwa katika mradi huu na Kampuni ya Tigo – Zantel ilipewa jukumu la kufikisha mawasiliano katika Kijiji hicho.
Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Wizara imeiagiza UCSAF kufika katika Kijiji cha Kandwi kufika wiki ya kwanza ya mwezi huu Septemba kwa lengo la kufanya tathmini ya kina ili kubaini kama kuna eneo lolote lenye changamoto ya mawasiliano liweze kutatuliwa.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved