Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Juma Usonge Hamad
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chaani
Primary Question
MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. JUMA USONGE HAMAD aliuliza: - Je, lini Serikali itatuma wataalamu kwenda Kijiji cha Kandwe kilichopo Wilaya ya Kaskazini Unguja ili kutatua changamoto ya mawasiliano?
Supplementary Question 1
MHE. JUMA USONGE HAMAD: Mheshimiwa Naibu Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwa majibu mazuri. Swali langu ni kwamba, je, ni lini mtaweka commitment ya kwenda kwenye Kijiji cha Kandwi ili kujionea hasa mazingira ambayo wananchi wangu wa Kandwi wanakosa huduma ya mawasiliano ukilinganisha na maeneo mengine?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kwanza nimpongeze Mheshimiwa Juma kwa ufuatiliaji mzuri, lakini naomba niliambie Bunge lako Tukufu kwamba tayari timu yetu imefika kwenye Jimbo lake eneo hili la Kandwi na tayari wameweza kuona changamoto ambayo ipo, hasa ni miembe mingi ambayo ipo katika lile eneo. Hata hivyo, kama Wizara, tayari tunafanyia kazi na kuhakikisha kwamba mapema iwezekanavyo tunakuja kuhakikisha maeneo haya ya Kandwi yanapata mawasiliano ya uhakika Mheshimiwa Juma.
Name
Festo Richard Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. FESTO R. SANGA K.n.y. MHE. JUMA USONGE HAMAD aliuliza: - Je, lini Serikali itatuma wataalamu kwenda Kijiji cha Kandwe kilichopo Wilaya ya Kaskazini Unguja ili kutatua changamoto ya mawasiliano?
Supplementary Question 2
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu kwa Wizara ya Habari, Mheshimiwa Naibu Waziri anakubaliana nami kwamba vitendo vya utapeli mitandaoni vimezidi? Je, Wizara ya Habari haioni haja ya kusitisha usajili wa laini kiholela mitaani hasa watu waende kujisajili kwenye maduka maalum ya hii mitandao ya simu kama nchi jirani wanavyofanya ili kudhibiti utapeli huu ambao umekuwa ukiumiza na kugharimu Watanzania wengi?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Festo Sanga kuhusu utapeli mitandaoni. Nampongeza sana kwa ufuatiliaji, lakini vitendo hivi vya utapeli tayari TCRA inaendelea kudhibiti na mojawapo, kwanza tume-restrict sana mikoani maeneo ambayo watu wanapata usajili sasa hivi siyo kila mahali. Kwa hiyo, tutaendelea kuona namna njema ya kuweza kuruhusu hawa wanaotoa huduma ya usajili tunaendelea kuwadhibiti.
Mheshimiwa Naibu Spika, hata kama tutaongeza scope ya kuona kwamba wanaweza kufikiwa, lakini vilevile kuhakikisha kwamba hali ya usalama na hali nzuri ya mawasiliano inaendelea kuboreshwa. TCRA wanafanya kazi nzuri sana katika hili.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved