Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 50 | Information, Communication and Information Technology | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 645 | 2024-06-20 |
Name
Jonas William Mbunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbinga Mjini
Primary Question
MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza:-
Je, ni lini Serikali itajenga minara ya simu katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga, ili kurahisisha mawasiliano?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Serikali kupitia UCSAF inatarajia kufikisha huduma za mawasiliano kwa kupitia mradi wa Tanzania ya Kidijitali (DTP) ambapo jimbo la Mbinga Mjini limenufaika kwa kupata minara mitatu. Minara miwili inajengwa na AIRTEL katika Kata ya Kitanda ambapo mnara mmoja umejengwa katika kijiji cha Utiri na ujenzi wa mnara wa pili uko katika hatua za mwisho. Vilevile Kampuni ya Simu ya VODACOM inatarajia kujenga mnara katika Kijiji cha Ruvuma Chini kilichopo katika Kata ya Mpepai. Baada ya kukamilika kwa minara hii Serikali kupitia UCSAF itafanya tathmini ya hali ya mawasiliano katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga na kuchukua hatua stahiki kwa maeneo yatakayokuwa hayana mawasiliano.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved