Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jonas William Mbunda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbinga Mjini
Primary Question
MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itajenga minara ya simu katika Halmashauri ya Mji wa Mbinga, ili kurahisisha mawasiliano?
Supplementary Question 1
MHE. JONAS W. MBUNDA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza naishukuru Serikali kwa kujenga minara katika Kata ya Kitanda na Kata ya Utiri. Nina maswali mawili ya nyongeza:-
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza. Nataka nijue ni lini sasa Serikali itakamilisha ujenzi wa Mnara wa Simu katika Kijiji cha Ruvuma Chini, Kata ya Mpepai?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Kata za Kikoro na Kagugu zina changamoto kubwa ya mawasiliano. Ni lini Serikali itatenga fedha, kwa ajili ya ujenzi wa minara katika Kata hizo?
Name
Maryprisca Winfred Mahundi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nakupongeza sana Mheshimiwa Mbunge Mbunda kwa namna unavyoendelea kufanya ufuatiliaji wa minara hii, mawasiliano ni muhimu sana.
Mheshimiwa Naibu Spika, eneo hili la Ruvuma Chini mnara huu tunatarajia ukamilike ndani ya wakati wa mkataba na katika kata hizi mbili alizozitaja tayari wataalamu wetu wapo kwenye site wanafanya survey. Kufikia Mwezi Disemba maeneo haya uliyoyataja ya Kikoro na Kagugu, Mheshimiwa Mbunda, tunakuja kujenga minara.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved