Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 15 | Sitting 9 | Information, Communication and Information Technology | Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari | 116 | 2024-04-18 |
Name
Mohamed Lujuo Monni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chemba
Primary Question
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza:-
Je, lini Serikali itajenga mnara wa Mawasiliano katika Kata ya Kimaha, Kijiji cha Mwaikisabi –Chemba?
Name
Nape Moses Nnauye
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtama
Answer
WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Lujuo Monni, Mbunge wa Chemba, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia UCSAF iliijumuisha Kata ya Kimaha katika Mradi wa Kufikisha Huduma ya Mawasiliano ya Simu uliosainiwa tarehe 13 Mei, 2023. Utekelezaji wa mradi huo unaendelea ambapo Mtoa Huduma Halotel anajenga mnara kwa ruzuku ya Serikali ya kiasi cha shilingi 145,000,000 za Kitanzania, kwa lengo la kuhudumia Vijiji vya Mwaikisabe, Chukuruma, Wisuzaje na Mwailanje. Mnara huo tayari umejengwa na kwa sasa mtoa huduma anaendelea na kazi ya kufunga vifaa vya redio. Mnara huu unatarajiwa kuwashwa mwezi Juni, mwaka huu. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved