Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mohamed Lujuo Monni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chemba
Primary Question
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga mnara wa Mawasiliano katika Kata ya Kimaha, Kijiji cha Mwaikisabi –Chemba?
Supplementary Question 1
MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri sana ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; maeneo ya vijiji vyote vinavyozunguka Mradi wa Bwawa la Farkwa, mradi mkubwa kabisa, Kijiji cha Sakaletwa, Gonga Chini na Gonga vyote havina mawasiliano. Naomba kujua ni lini sasa, Serikali itajenga mnara katika maeneo ya mradi ule unaoendelea ili wafanyakazi wote walioko pale wapate mawasiliano?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili; Kijiji cha Magasa wataalamu walifika wakaainisha eneo la kujenga mnara, lakini mpaka leo hawajarudi. Naomba kujua ni lini sasa watarudi ili kuendelea na kazi ile? Ahsante.
Name
Nape Moses Nnauye
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtama
Answer
WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Monni, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba, eneo la Mradi mkubwa wa Bwawa la Farkwa kwenye vijiji alivyovitaja vya Sakaletwa, Gonga na Gonga Chini kuna mahitaji makubwa ya huduma za mawasiliano. Wataalamu wetu walishafika eneo hili na wamefanya uchambuzi na taarifa zipo Wizarani, utaratibu unaendelea kwa ajili ya kuwapatia huduma za mwasiliano kwenye eneo hilo.
Mheshimiwa Naibu Spika, pia Kijiji cha Makasa alichokitaja ni katika vijiji ambavyo viliingizwa kwenye mradi ule wa minara 758 na UCSAF waliingia makubaliano na TTCL na tayari walishalipa hela ya awali na wamesaini. Kwa hiyo, kazi itaanza hivi karibuni, wamesaini mkataba huo Mwezi Machi na huu Mwezi Aprili mwishoni kazi itaanza. (Makofi)
Name
Munde Abdallah Tambwe
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga mnara wa Mawasiliano katika Kata ya Kimaha, Kijiji cha Mwaikisabi –Chemba?
Supplementary Question 2
MHE. MUNDE T. ABDALLAH: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa fursa niulize swali la nyongeza. Tabora Manispaa katika Kata ya Malolo, Kijiji cha Usenge, hakuna kabisa mawasiliano ya simu. Je, Mheshimiwa Waziri anatupa action plan gani ya kuhakikisha ametuwekea mnara kwenye kata hiyo ya Malolo? (Makofi)
Name
Nape Moses Nnauye
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtama
Answer
WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Munde, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Munde, tulipoenda Tabora alikuja kutuona na akaleta malalamiko ya eneo hili. Pia nimhakikishie barua yake aliyotuandikia ya eneo hili husika tumeipokea na tunaifanyia kazi na namuahidi wataalamu wameshafanya utafiti na eneo hili litapatiwa huduma za mawasiliano hivi karibuni. (Makofi)
Name
Flatei Gregory Massay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga mnara wa Mawasiliano katika Kata ya Kimaha, Kijiji cha Mwaikisabi –Chemba?
Supplementary Question 3
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwanza nimshukuru Rais kwa kujenga minara Mbulu Vijijini. Je, Mheshimiwa Waziri lini tutaambatana kuizindua ile minara?
Name
Nape Moses Nnauye
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtama
Answer
WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, minara mingi kwa sasa imekamilika katika maeneo mengi na mpango ilikuwa minara zaidi ya 250 ingewashwa wakati wa Sherehe za Muungano. Kwa hiyo, tutaangalia ratiba na kwa sababu hapa siyo mbali, tutapanga mimi na yeye, tutakwenda kukagua na wataalamu wetu wakiridhika tutawasha hiyo minara ambayo imekuwa tayari. (Makofi)
Name
Dennis Lazaro Londo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mikumi
Primary Question
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza:- Je, lini Serikali itajenga mnara wa Mawasiliano katika Kata ya Kimaha, Kijiji cha Mwaikisabi –Chemba?
Supplementary Question 4
MHE. DENNIS L. LONDO: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujua kauli ya Serikali kuhusiana na suala zima la ukamilishaji wa minara ya mawasiliano katika Kata za Vidunda, Kisanga, Uleling’ombe, Kilangali na Malolo?
Name
Nape Moses Nnauye
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mtama
Answer
WAZIRI WA HABARI, MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, maeneo aliyoyataja itabidi ni-cross check kuona kwamba hayamo kwenye Mradi wa Tanzania ya Kidijiti unaoendelea. Kama hayamo nitoe ahadi Mheshimiwa Rais Samia ameshatutengea fedha kwa ajili ya minara mingine zaidi ya 600, ambayo nayo tutaigawanya kwenye maeneo ambayo hayakuingia kwenye Mradi wa Tanzania ya Kidijiti.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved