Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 2 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 30 | 2024-08-28 |
Name
Mashimba Mashauri Ndaki
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Magharibi
Primary Question
MHE. MASHIMBA M. NDAKI aliuliza:-
Je, Serikali inachukua hatua gani kuhakikisha kuna ushindani miongoni mwa wafanyabiashara wanunuzi wa zao la pamba nchini?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-
Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Serikali inaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha mifumo ya ununuzi na kuhakikisha kunakuwa na ushindani katika ununuzi wa pamba kwa mujibu wa sheria na miongozo ya biashara ya zao la pamba.
Mheshimiwa Spika, ununuzi wa pamba nchini hufanyika kwa utaratibu wa soko huru ambapo zaidi ya kampuni 35 zimesajiliwa na kupewa leseni ya kununua pamba na usajili unaendelea ili kuongeza ushindani. Kampuni hizi hununua pamba kulingana na hali ya soko ya msimu husika na bei dira iliyokubaliwa na wadau. Aidha, Serikali husimamia na kuhakikisha bei dira iliyokubalika na wadau inazingatiwa katika ununuzi wa pamba.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved