Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mashimba Mashauri Ndaki
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Maswa Magharibi
Primary Question
MHE. MASHIMBA M. NDAKI aliuliza:- Je, Serikali inachukua hatua gani kuhakikisha kuna ushindani miongoni mwa wafanyabiashara wanunuzi wa zao la pamba nchini?
Supplementary Question 1
MHE. MASHIMBA M. NDAKI: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kampuni hizi zinapofika ngazi ya wilaya au kata yanagawanywa kwenye kata moja, mbili au tatu na hivyo kutengeneza ukiritimba kwenye hilo eneo. Yaani kampuni moja inanunua pamba kwenye hilo eneo na kufifisha sasa ushindani ambao tuliutarajia. Je, Serikali inatoa tamko gani kuhusiana na tabia ya namna hii? Ahsante.
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, moja ni kwamba wanunuzi wote wenye leseni wanaruhusiwa kununua pamba eneo lolote isipokuwa katika kesi ambayo anaeleza Mheshimiwa Mbunge ni kwamba kulikuwa na kampuni ambazo zilielekeza katika kata kama 40 kama case study ili kuweza kujifunza namna ambavyo wamefanya uwekezaji katika pamba ikiwemo kutoa pembejeo kwa wakulima wa pamba. Kwa hiyo wakaruhusiwa vilevile kununua katika maeneo hayo.
Mheshimiwa Spika, tamko la Serikali ni kwamba, maeneo yote ambayo wanunuzi wote wamepewa leseni wana haki sawa ya kununua pamba. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved