Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 16 | Sitting 7 | Community Development, Gender and Children | Wizari wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto | 112 | 2024-09-04 |
Name
Esther Edwin Maleko
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ESTHER E. MALLEKO aliuliza:-
Je, upi mkakati wa kupata hatimiliki maeneo yanayomilikiwa na vituo vya wazee, watoto na taasisi za ustawi na maendeleo ya jamii?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMIII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara inayo mikakati mbalimbali ya kuhakikisha kwamba vituo vya huduma za ustawi wa jamii na shughuli za maendeleo ya jamii vinapata hatimiliki za ardhi. Moja kati ya mikakati hiyo ni kutenga bajeti, ambapo katika Mwaka huu wa Fedha 2024/2025, Wizara imetenga shilingi milioni 75.7 kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli hizo.
Mheshimiwa Naibu Spika, kati ya vituo 29 vya Wizara, vituo 15 vimefanikiwa kupatiwa hati miliki na maeneo mengine 14 yapo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa upatikanaji wa hati hizo. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved